Nguvu Halisi Iliyopo Ndani Ya Mwanadamu
Hello.....
Karibu tena kwenye blog yangu, karibu tena kwa ajili ya kujifunza, na baada ya kusoma kama utakuwa na swali..utaliandika kwa kuandika ujumbe wako chini ya hii post...
Barikiwa sana
Kama
vile ambavyo binadamu huitaji chakula ili apate nguvu…na nguvu hiyo huitumia
kufanya mambo mengine ya kiroho na kimwili pia…
Vivyo
hivyo kwa upande mwingine.. uhai wetu umeshikiriwa na vitu vitatu
Mwili, Nafsi na Roho
Na
ili tuwe hai kamili.. vitu vyote vitatu vinahitaji kulishwa, kutunzwa na kukua,
kama vile mwili ukuavyo, mti ukuavyo nk….
Mwili
yeye hula chakula cha mwilini, ugali wali nk, nafsi yenyewe huishi kutegemeana
na yale tunayowaza na kufikiria ambayo chanzo chake ni milango ya fahamu katika
mwili mazingira..…
Roho
yenyewe hula chakula cha rohoni…kwa mfano neno la Mungu..maombi..nk
Mtu
huru yule ambaye mwili wake, nafsi yake na roho yake vinaenda sambamba, maana
yake ni hivi, mwili wake unatenda kile ambacho nafsi yake unakishuhudia na
nafsi yake inatenda kile ambacho roho inakishuhudia….
Maana
yake ni nini........
Maana
yake ni kwamba kile kinachodhihirika nje ya mwili ndicho kilichopo kwenye nafsi
na roho yake….
Mtu
huyu hatojuta hata siku moja katika kila anachokifanya..maana anachokifanya ni
matokeo ya umoja wa mwili, nafsi na roho..
Vitu
hivi vitatu visipokwenda sawa inasababisha vitu vifuatavyo..
Woga,
hofu kutokujiamini na kukosaa ujasiri, kuwa na maswali mengi yasiyo na majibu..
Tusome maandiko ya Mtume paulo, Warumi 7:15-25 namna alivyopitia hali ya mashindano kati ya mwili nafsi na roho yake.
''Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu. Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya kazi mwilini mwangu.
24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo? 25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria ya dhambi.
Hivyo hapo tunajifunza, Asili ya mwili ni dhambi na uovu, na namna pekee ya kuutiisha mwili ni, kuilisha nafsi kile unachotaka kitokee na roho ambayo ina asili ya uungu ili viweze kuwa na nguvu ya kuuongoza mwili.
Ambayo
hayo yote husababisha kupungua kwa nguvu ya ndani ya mtu halisi…
Kwahiyo
vitu hivi vitatu lazima viwe na mawasiliano hatakama kutakuwa hakuna chakula
cha kila mmoja, lazima vyote uvipe taarifa kwamba leo nafsi hautokula.. au
mwili hautokula au roho hautokula leo..
Kizazi
chetu cha leo kimekuwa kikishindwa kujua namna ya kuviendesha hivi vitu vitatu,
na hivyo imepelekea watu wengi kufa kimya kimya…yaani mwili u hai lakini roho
imekufa, au
unakuta mwili upo nafsi imefungwa na roho inalalamika (unakuwa mateka)
Na
mwingine roho ipo kivyake, mwili kivyake, alkadharika na nafsi
kivyake na wengine wameingiwa na roho zingine, ambazo zimesababisha nguvu ya roho halisi kutokuonekana..kwasababu ya kushindwa kuviendesha hivi vitu vitatu kwa maana nyingine ni kuwa mateka kama mtume Paulo anavyosema. ……
Mwili
hufuata roho kama tu roho atakuwa na nguvu maana yake nini….roho akiwa
ameshiba, au kama anachochote kitu, mwili utaladhimika kuifuata roho ambayo
mara zote hutoa taarifa ambazo ni sahihi na za kiroho..
Lakini
endapo ikitokea roho hana nguvu, mwili hautoweza kusimama peke yake, utaitafuta
nafsi kwa ajili ya support,
Na
kama tujuavyo nafsi hua na nguvu kutokana na mazingira ya nje ya mwili ambayo
huingia ndani ya nafsi kupitia milango ya fahamu…
Na
baada ya hapo, mazingira yale hujitengenzea mfumo wa kutawala ambao mfumo huo
huipa nafsi nguvu ya kumiliki mfano kutafuta inspirational quotes videos,
marafiki ambao utahisi lazima watakuunga mkono,hizo ndo tunaziita nguvu za
ziada, kwahiyo katika wakati huo mwili utafata yale ya kwenye nafsi.
Kumbuka
roho ni pumzi ya Mungu… maana yake ni mali ya Mungu..kwahiyo roho ikishindwa
kuendesha mwili asili ya uungu inapungua ndani ya mwanadamu
Kwahiyo
nafsi hua inapata nguvu wakati roho ikiwa imekosa nguvu, na baada ya hapo nafsi
hujitengenezea makoloni yake kwa kutafuta nguvu kutoka nje ya mwili kupitia
milango ya fahamu (nimetoa mifano hapo juu)… ili mwili uendelee kufanya kazi na mtu aendelee
kuishi..
Nafsi haijali mtu ataishi katika mazingira gani, muhimu ni mwili uishi…
Na
kwanini nafsi itengeneze mfumo wake wa utawala binafsi… ni ili kuleta balance
kwasababu roho wakati haina nguvu nafsi itatakiwa kubeba nafsi ya roho.. ili mwili
uendeshwee…
Sijajua
hadi sasa umejifunza nini, lakini katika maisha yako ya kila siku, maamuzi yako
yanapaswa kuwa sambamba katika vitengo vyote vitatu ambavyo ni mwili nafsi na
roho,,
Kitu
ambacho mwili unafanya na roho inakataa usikipe nafasi.
Kitu
unacho kiangalia na kikaondoa Amani ya roho Usikiangalie tena
Maamuzi
uliyofanya yakayokuweka mtumwa, achana nayo…
Ingawa
Mungu hakuonekana dhahiri katika macho yetu lakini alishaweka mfumo wa utambuzi
ndani yetu,,ameweka mfumo wa mawasiliano ndani yetu tayari..
Roho
lazima iwe juu ya vyote, tumia muda kuipa roho nguvu juu ya mwili na nafsi.
Mfano
tu..
Utakuta
maisha ya mchungaji au mwalimu au muhubiri ni tofauti na hayo anayoyahubiri au anayoyafundisha
…sababu ni mwili roho na nafsi …au kwa lugha nyingin ni kwamba roho ipo mbali
na nafsi na mwili..maana yake mtu huyo ameupa nafasi mwili na nafsi.
Kuwa
na uhakika wa maamuzi unayoyafanya lazima kwanza uwe na uhakika wa uwepo wa
mawasiliano mazuri kati ya mwili, nafsi na roho,
Lakini
cha muhimu Zaidi ni kuongeza nguvu ya roho (kuilisha roho kwa neno la MUNGU),
ili nafsi na nguvu za nje ya mwili zisipate nafasi.
Kizazi
chetu cha leo kimekuwa kinaishi yale yanayosemwa na si yale yatokayo ndani yao.
Wanaishi wanayoyaona na si yale ambayo
ni matokeo ya Imani zao za ndani..
Na
hii imesababisha uwepo wa maswali mengi juu ya Imani na matendo yao, hofu
nyingi katika kila wanalolitenda.
Hawahitaji
ushirika na roho mtakatifu na badala yake wanamuhitaji mwenye ushirika na roho
mtakatifu..
Wana
Imani lakini bado hawaamini. Wamekuwa watumwa wa Imani zao.
Yesu
alisema utaijua kweli na hiyo kweli itakuweka huru, lakini ukija kuangalia watu
wengi tunaujua ukweli lakini hatuko huru..
Maana
yake nini kuna siri ndani ya iyo kweli ambayo kila mmoja anapaswa kuitambua kwa
uwezo wa roho mtakatifu ili awekwe huru.
Shida
kubwa tuliyonayo ni kwamba, hatujui nguvu au uwezo uliopo ndani yetu, na namna
ambavyo ukiufanyia kazi vizuri utaweza fika popote unapotaka ili kutimiza ndoto
zako.
Your
Future is within yourself..
Uwezo
wa Kujua usahihi wa yale tunayoyafanya uko pia ndani yetu..
Uwezo
wa kujua huyu ndiye, huyu sie pia upo ndani yetu..
Lakini
kwasababu hatujui ndomana tunakosea sana kutafuta nguvu nyingine nje na kusahau
iliyopo ndani yetu..
Tafuta
kujua nguvu na uwezo uliopo ndani yako kila siku..
maana hata sasa hakuna aliyejua uwezo wote alionao ndani yake, lakini tunakavyovijua ndivyo hivyo tunafanyia kazi.
Jifunze
namna ya kuendesha hisia zako, mawazo, kuifunza akili yako kwa kuipa vitu
unavyoona unavyovihitaji au utakavyovihitaji..
Kuwa
msikilizaji sana kuliko kuwa muongeaji..
Fikiri
sana kabla ya kutenda.
Focus
yourself on building strong foundation of your own faith, to the point that you
can stand and defend it, to the point that no one will shake you.
Itaendelea…
Asante Sana Kwamafundisho yako manzuri
ReplyDelete"Shida kubwa tuliyonayo ni kwamba, hatujui nguvu au uwezo uliopo ndani yetu, na namna ambavyo ukiufanyia kazi vizuri utaweza fika popote unapotaka ili kutimiza ndoto zako." Angel Fabian quotes
Asante Sana
ReplyDelete