Posts

Showing posts from July, 2018

MAISHA NA TANZANIA

Maisha ni mkusanyiko wa matukio vipindi vyote vya maisha ambavyo mtu binafsi ameweza kuvipitia tangu alivyozaliwa mpaka sasa alipo na umri aliokuwa nao Kuishi katika jamii na aina ya watu wa kitanzania kumenipa maana hiyo ya maisha...nikimaanisha kwamba kila mtu ana maana yake na jinsi yake ya maisha... Imenifundisha kuwa kila mwanadamu ana maisha yake...ambayo ni tofauti na mwingine na ndio hapo utapata mitazamo tofauti juu ya maisha... Inanipa wakati mgumu sana kufikiri jinsi gani unaweza kuishi maisha yako kwenye jamii ya watu zaidi ya milioni ambao kila mtu pia anaishi maisha yake.... Kuna watu ambao Mungu amewapa neema ya kutoonja hata tone la shida tangu wamezaliwa hadi kufa...na kuna wengine sio tu kuonja ...ila wanapata shida tangu mwanzo wa kuzaliwa au mwisho wao na ndio hao watumishi wazuri wa Mungu... Kuna wengine wanafanikiwa sana kimasomo...ila kuna wengine wanakesha usiku kucha kusoma lakini hawafanikiwi... Kuna wengine wanapata shida pale tu wanapokari