Posts

Showing posts from September, 2018

YESU NA KANISA LETU

Nilienda siku moja katika kanisa moja kubwa sana lenye kufahamika sana jijini Dar es salaam, Ilikuwa ni mara yangu ya pili mimi kukanyaga katika lile kanisa baada miaka  mingi kupita, kanisa lilifurika watu wengi jumapili ile, na watu wengi walionekana kuwa na shauku ya kupokea miujiza yao... Nyuso za watu wengi zilionyesha kukata tamaa na kuchoshwa sana na hali ya ugumu wa maisha, Wengine waliwaleta wagonjwa wao pale kanisani na wengine walikuja kwa ajili ya kutatuliwa matatizo yao binafsi..... Madhabahu ya kanisa lile ilikuwa nzuri na ya kupendeza, vitambaa vyake vilikuwa vikimetameta, ilikuwa ni raha sana ukiangalia madhabahu ile, na ukiangalia hata wahudumu walikuwa wamevalia mavazi mazuri ikiashiria uzuri wa hali za maisha yao. mchungaji mkuu alivalia vazi zuri kubwa la kumetameta kiasi kwamba alikuwa akionekana kanisa zima hata ukiwa mbali.. Ibada iliendelea waimbaji wazuri waliitwa wakaimba watu wakafarijika na kufurahi sana ile siku Basi mchungaji akapanda madh