IT WILL BE JUST FINE.

       Maisha ni mkusanyiko wa matukio mengi ambayo dhamira yake ni kutufundisha, kuturekebisha ili tufike katika hatima zetu ambazo Mungu ametupangia.

       Lakini maisha haya yamejaa mitego na mafumbo mengi ambayo wengi wetu tumeshindwa kuitatua, ni kama mafumbo kwenye hisabati, ukipata thamani ya X itakusaidia kupata thamani ya Y, na wakati mwingine thamani ya X na Y itakusaidia kupata thamani ya Z.

Mafumbo haya yanahitaji, utulivu, uvumilivu, hekima subira imani na maarifa na mengine mengi ili kuweza kuyavumbua.

                                                Mungu atusaidie

This is my before.                                                                            Nimekuwa mtu wa kila aina, kwa kipindi kichache nilichoishi, na kwa asilimia kubwa nimekua mtu wa kuogopa sana, hasa katika maswala yanayohusu maisha yangu.

kila asubuhi yangu, ilianza na maswali mengi sana, kwamba leo itakuwaje, what if nikafanya kazi nisipate ela, itakuwaje kama nisipolipwa pesa zangu, leo sina ela ntaishije...
Hofu na mashaka kila iitwapo asubuhi., itakuwaje nisipopata kazi..itakuwaje kama biashara isipoenda vizuri, itakuwaje nikikosa, au nikipata itakuwaje...
Na wakati mwingine nimekutana na changamoto zilizomaliza mafuta kwenye mwili wangu na kushusha kiwango cha imani yangu..

Mungu alinipa, but i needed more and more (kutokuridhika), na kusahau kushukuru.

This is Me now..
Am not successful enough to convince you, lakini ninayo furaha kubwa, kufanikiwa kuishi maisha marahisi, yanayobeba shuhuda kila siku..

Unapokuwa hutumii nguvu, katika kufanikisha mambo yako, unapoona Mungu anakupa mahitaji yako, na kuondokana na muda wa kuwa na hofu
Unapoona hofu inakujia, au uwoga, muda huo huo shift it to God.. let your heart be free
     
You dont know the secret... let me tell you..

NGUVU YA KUPANDA UNAYO..LAKINI HUNA NGUVU YA KUKUZA
UNAWEZA UKAWA NA NGUVU, UKAKOSA UWEZO..
NI KWELI KWAMBA UTAVUNA ULICHOPANDA, BUT TRUST ME KUNA WATU WANAVUNA  AMBAVYO WALIPANDA WENGINE. 
NA WENGINE WALIPANDA NA HAWAKUVUNA.

Kujifunza kumwachia Mungu nafasi katika maisha yako ndio siri

I chose to believe there is only one God, who created us, and the universe, and everything, he created us with purpose and he knew how to make it be done.. he prepared the way, he showed us the way, its us now to decide to follow...

Nimejifunza kuishi kwa imani...na imani hiyo ni moja tu, YEYE ALIYE IANZISHA SAFARI NA ATAIMALIZA...
Nimejifunza katika hali zote kuacha Mungu achukue nafasi yake, na kuomba na kulia sana ili niweze kufika katika hatima aliyoniandalia..

Nimejifunza kuaapreciate uumbaji wa Mungu, kwa viumbe wake... na kuona kwamba sisi sote ni binadamu walewale..

Na kwamba sisi sote ni watu..

Nimejifunza kuomba msamaha, na kuona kwamba binadamu anaweza kukosea, kuona uzuri wa mtu mbaya pia nimejifunza..

Maana niliwaona watu ambao hawana kabisa, alafu pia nikawaona na waliokuwa navyo..na wote nikawaona ni watu walewale

NA katika vitu vingi nilivyokuwa na hofu navyo, nilivipata na vikapita..sikuvipata kwa nguvu zangu, na ndio hapo nikasema sitasumbua ubongo wangu.

Utakapopita katika njia ngumu sana, wala usikimbilie mbali, Yupo yule aliyekuumba, nenda ukamuachie mzigo wa maisha yako..

Maana tulipita katika changamoto nyingi, lakini embu angalia, leo hazipo tena na hata pengine hatuzikumbuki..

Furahi kwasababu na wewe unapitia hizo changamoto, ambazo kesho tutaziita shuhuda...
Maana hakuna jipya chini ya jua..
 
Tazama katika yote yale, maisha yaliendelea, na mengine sijui yaliishaje lakini yaliisha 
                
                  YOTE YATAPITA NA KILA KITU KITAKUWA SAWA..
                                                     KABISA...

                                                Be blesses y'all





Comments

Popular Posts