Mungu wa Agano
πUumbaji
Kabla ya Mungu kumuumba Mwanadamu, kuna namna alimuandalia mazingira mazuri, kwa namna kwamba kila kitu ambacho mwanadamu angekihitaji kilikuwepo bustanini,
Soma Mwanzo 1: 28-31, "Ikawa hivyo. Basi, Mungu akafanya aina zote za wanyama wa porini, wanyama wa kufugwa, na viumbe vitambaavyo. Mungu akaona kuwa ni vyema. Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.” Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya sita."
Lakini turudi kwenye sababu kwanini Mungu alimuumba Mwanadamu,
Soma mwanzo 2:4-5,7, Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima.Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Basi, Mwenyezi-Mungu akamtwaa huyo mwanamume, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Ukisoma vizuri utaelewa kwamba, Mungu alimuumba mwanadamu kwa lengo la kuilima na kuitunza Bustani, lakini katika kulitimiza hilo alimpa mamlaka ya kutawala, kumiliki na kumtaka aongezeke ili kuijaza bustani.
Na katika uumbaji wote Mungu aliyoufanya, yote aliyaona kuwa ni mema na yanafaa..
πBwana akaghairi kwakuwa alimfanya Mwanadamu
Ukisoma Kitabu cha Mwanzo 6:6 Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake, hivyo akasema, “Nitamfuta kabisa duniani binadamu niliyemuumba; nitafutilia mbali pia wanyama wa porini, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Ninasikitika kwamba niliwaumba duniani.”
Kusudi la Mungu hapo awali lilikuwa jema na zuri, lakini kwa mwanadamu ilikuwa tofauti, uovu uliongezeka soma Mwanzo 6:5, uovu ulikuwa mkubwa na kupelekea Bwana kughairi makusudi yake kwa Mwanadamu
Kutoka hapo tunaona Mungu alianza kufanya kazi na mtu mmoja mmoja ambaye anakubali kufuata maelekezo yake, na Mungu anafanya agano naye huyo, na kusimamia agano lake
πNoah
1. Alionyesha utayari wa kumtumika Mungu, biblia inatuambia alikuwa mtu wa haki na mkamilifu katika vizazi vyake, tabia hiyo ilimpatia kibali na kupata neema machoni..( Utayari) soma Mwanzo 6:9
2. Mungu akafanya agano nae; Mwanzo 6:18
3. Mungu anambariki Noah na uzao wake, Mwanzo 9:1
πAbraham
1. Bwana alianza kuongea na Abraham kwa kumpa maelekezo, na tunaona Abraham akakubali kumsikiliza Mungu, ( utayari) soma Mwanzo 12:1,4
2. Mungu anatoa ahadi kwa Abraham baada ya Agano. soma Mwanzo 12:2,3
3. Mungu anambariki Abraham kwa utajiri wa fedha, mifugo na dhahabu. soma Mwanzo 13:2
π Isaka
1. Bwana alimpa Isaka maelekezo na kumwambia akae katika nchi ambayo atamwambia, na isaka akakubari (utayari) soma mwanzo 26:2,6
2. Bwana anampa ahadi za kumbariki Isaka kama atakubali kutembea nae (agano), Mwanzo 26: 3,4
3. Mungu anambariki Isaka baada ya kukubali kutembea nae. Soma Mwanzo 26: 12-14
π Yakobo
1. Mungu anafanya agano na yakobo na kumuahidi kutembea nae. Soma Mwanzo 28: 11-15
2. Yakobo anaweka nadhiri kwa Mungu (utayari). Mwanzo 28:20
3. Malaika alimbariki na kumshindia katika vita zake zote.
Kwahiyo kwa ujumla tunajifunza mambo yafuatayo;
1. Mungu anataka kutembea na wewe anataka kufanya agano na wewe, ili upate kubarikiwa na baraka zote za rohoni na mwilini, kubali kutembea na Mungu, kutii na kuisikiliza sauti yake na kufuata anayokuelekeza ndipo baraka zitakapokujia
2. Mungu anaheshimu maagano, ni Muhimu kuweka agano na Mungu, ili hata wakati wa udhaifu Mungu akushindie kupitia agano lake.
3. Mungu ametupa nafasi nyingine 2026, tengeneza mahusiano yako na Mungu ili upate kuhesabiwa na wewe kuwa miongoni mwa wanufaika wa Baraka za rohoni.
2026 ANZA BWANAππ
Comments
Post a Comment