2025 Life Lessons
Hellow, Habari..
Karibu katika ukurasa wangu, leo nitashare vitu nilivyojifunza mwaka 2025.
1. Umuhimu wa kutambua wewe ni nani, na unataka nini na unataka ufike wapi.
Nimeona dunia inatoa options nyingi za mtu kuchangua, na kuna wakati ina recommend nini uangalie au nini ufanye, lakini pia kuna watu mbalimbali wanakuona unafaa kwenye maeneo fulani...lakini mwisho wa siku wewe ndio unapaswa kufanya maamuzi ya nini ufanye na nini usifanye kulingana na unachokitaka.
Kuwa na kitu unachokitaka, au nnaweza kusema kuwa na malengo, alafu fanya tathmini ya nini au nani unamuhitaji ili uweze kupata unachokitaka au uweze kufikia malengo yako.
2. Focus na unachokitaka.
Vijana wengi tumekuwa na mipango mingi ambayo haitimii, leo unapanga hili kesho unafanya lingine, kesho unapanga lingine hili halijaisha unajaribu lingine.
Kitu nilichojifunza ubora unatokana na uzoefu, pale ambapo mtu anachagua kitu na anawekeza katika hicho hadi kinasimama na kuwa bora zaidi, hivyo consistency ni muhimu katika kuwezesha mafanikio katika mipango yako..
Stick to the plan, uthabiti (consistency) lakini pia kutokukata tamaa na uthubutu.
3. Watu huja na kuondoka katika maisha yako, na asilimia kubwa ya watakao kuja kwenye maisha yako wanategemea kubenefit kwa namna mbalimbali. kwahiyo jitengenezee mtazamo wa kutokuendeshwa na kutokutegemea watu. Ruhusu watu kuja na kuondoka na hata kubaki kama wataona umuhimu wako kwao.
4. Nguvu ya kukaa Kimya na kusikiliza.
Katika kuishi nimegundua watu wana mitazamo tofauti tofauti, na kila mmoja anatamani kukubalika katika kile anachokiamini kuwa ni sahihi..kwahiyo sio lazima kila mtu akubaliane na mtazamo wako, kuna wakati utahitaji kujifunza, kusikiliza na wakati mwingine kukaa kimya..
Kukaa kimya kunaongeza uono lakini pia inaongeza maarifa lakini pia inakupa nafasi ya kufikiri kabla ya kufanya maamuzi na kusikiliza vivyo hivyo.
5. Kukomboa wakati.
Ni ngumu kuelewa hii, kama unategemea kulipwa mshahara mwisho wa mwezi. lakini tujaribu kujifunza kwa waliofanikiwa namna wanaendesha maisha yao na kila dakika kwao ni pesa.. tujaribu kumhoji aliyesema ''time is money" hata biblia imetuambia kuhusu kuukomboa wakati.
soma waefeso 5: 16-17
''Mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.''
Usiwekeze muda wako kwa vitu au watu ambao hawakusaidii kufika malengo yako. muda wote unapaswa kujiuliza kwamba unachokifanya kina matokeo au manufaa gani kwenye malengo yangu..
6. God loves us, indeed he does.
Imagine mwaka mzima, upo mzima umepiga hatua, familia yako ipo salama, umemfanyia nini Mungu, imagine mara ngapi umemkosea kwa kujua kabisa kwamba unachofanya ni kosa, lakini angalia bado anakulinda, bado amekuepusha na mabaya, bado unakupa furaha, angalia maisha unayoishi tazama bado upo hai...bado ametupa nafasi..
Kuna wakati tunamsahau, kuna wakati hatumuamini, lakini angalia bado yupo na wewe..tazama..tujifunze kumpenda Mungu..
# 2026 usikubali kubaki pale ulipo
Comments
Post a Comment