WAKATI WA KUZAA MATUNDA (TIME TO BEAR FRUITS)

 

WAKATI WA KUZAA MATUNDA

(TIME TO BEAR FRUITS)

 

YOHANA 15:1-5

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima, kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu name ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.”

Tuanze na neno matunda.. ni matunda gani kristo alikuwa akiyanzungumzia

Mungu alitupa kazi moja tu, Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wake (Mathayo 28:19) , Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe (Marko 16:15)

 

MATUNDA..NI (kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa krisro, kwa njia moja tu ya kuihubiri injili.

Ni wajibu wa kila muamini kuihubiri injili ya Kristo kwa namna yoyote ile, ili mradi dhamira kuu iwe ni kumtangaza kristo

Majira haya sasa, tumejivua majukumu, mchungaji yupo atahubiri, padre yupo atahubiri, akihubiri mwakasege inatosha. Mwalimu yupo atafundisha.. ni kana kwamba hatujui wajibu wetu kama wakristo katika kujenga ufalme wa Mungu.

Tumekuwa wafuasi wasiokomaa wakafunza na wengine. Sisi ni wakufundishwa tu kila siku…

 Nikukumbushe tu.. kwamba kila tawi lisilozaa litakatwa kiufupi ni kwamba utawekwa nje ya ufalme.

Wewe unayemjua kristo, au umepata kujua kitu chochote ambacho kinaweza kutumika kujenga ufalme wa Mungu, USILALE, tumia hicho. Kwa ajili yako pia na kizazi chako.

Beba hilo kama ndio sababu ya wewe kuishi ( kusudi la maisha yako), sio kwamba uwe kiongozi au uwe nabii au uanzishe kanisa au upate watu wengi, hapana, hiyo ni sehemu ya maisha yetu..

Tumeona mambo mengi yakiharibika, lakini tumekuwa wakwanza kulaumu, na kusahau kwamba, tulipewa mamlaka ya kuunda na kubomoa, mbinguni na duniani, na  pengine hatujui kwamba mafanikio ya mwanadamu hayategemei mazingira ya kidunia.

Kiufupi tumejisahau

Tuko busy making money, tule, tujenge, twende shule, tupendeze, tununue magari, tumesahau kwamba katika yote hayo hatuwezi bila yeye..

Kwani ni wangapi, walienda shule na bado hawakufuraia, wenye pesa na bado wana shida..wenye vyakula na bado wana njaa..muhubiri akasema yote ni ubatili..

 

Ni afadhali ukaweka hazina yako mahali pasipoharibika.

Ni wakati wa kuzaa matunda… time to bear fruits

                                                            BARIKIWA

🙏

  HAPPY NEW YEAR

Comments

Popular Posts