I lost My identity.....
Ubinadamu umekuwa bora sana hasa kwenye karne hii, na wakati kama huu, kwa namna vile Mungu ametuumba, na kutupa kitu kiitwacho kumbukumbu..
Neno hili kumbukumbu limekuja kutokana na uwepo wa neno kusahau. Kila aliye binadamu anaweza kusahau na pia kukumbuka.
Hali
hii au tabia hii ya kusahau na kukumbuka imepelekea neno ubinadamu kuwa na
nguvu na ikapelekea kuwepo na sababu za kibinadamu.
Leo hii nimeshangazwa sana na uwepo wa uhalisia wa neno hili “I lost my identity” kwenye maisha yangu
Unaweza sema labda linatokea kwa wagonjwa wa akili au watu pengine waliochanganyikiwa la hasha, neno hili limethibitika kutokea hata kwa mtu wa kawaida ambae hana tatizo lolote pale tu anaposhindwa kujua vitu flani flani.
ππππππππ
ππWengi
wetu tunafahamu kwamba ni rahisi mtu kusahau kitu pengine alichokihifadhi au
labda kusahau kumpigia mtu simu au kutuma massage na kadhalika, lakini ni
vigumu sana kwa wengi wetu kusahau wao ni nani…
Nitatoa
mfano..
Je
umewahi kusahau jina lako…?
Je
umewahi kusahau kipaji chako, au kazi yako, au tu mahali unapofanyia kazi?
Bila shaka kwa namna ya kawaida ukiondoa matatizo ya kiafya ni vigumu sana kwa mtu kusahau vitu hivyo..
Sasa
leo makala hii ni kukuhabarisha juu ya uwepo wa uhalisi wa neno hili “I lost my
identity” na kwamba linaweza tokea kwa mtu yoyote, au kwa namna nyingine linaweza kutokea kwako pengine katika sura nyingine.
Mungu
alimuumba mwanadamu kwa namna ya kipekee sana, kila iitwapo leo humtengenezea
tumaini jipya kwa lengo la kumpa nguvu.
Lakini kwa bahati mbaya mwanadamu huyo akiwa mbali na uwepo wa Mungu, hapo ndipo itakapomlazimu yeye kujitengenezea tumaini litakalomtia nguvu ndani ya siku…. Na endapo tumaini hilo likikosekana mwanadamu huyo hufa katika nafsi yake
Tumaini
analolitoa Mungu ni tofauti sana na tumaini ambalo mwanadamu hujitengenezea,
Mungu humpa mwanadamu tumaini kwa kumpa nguvu na imani ndani ya roho yake na nafsi, humpa mwanadamu subira na uvumilivu.
Tumaini ambalo mwanadamu analitengeneza ni katika kujaribu tu kuzuia maumivu yasije, na kama yakija azime taa alale. Ni kama tu kutuliza tumbo lenye njaa wakati wa usiku, hali ya kuwa kuna asubuhi yaja. Lengo la tumaini hili ni kujaribu tu kuficha uhalisia wa ukweli wa Maisha..
Hapo nimejaribu tu kidogo kukwambia namna au asili ya hili neno “I lost my identity” linapoanzia na namna linaweza kuwa halisi kwako kuanzia ndani yako.
Kuna vitu muhimu vinaweza kuleta tumaini kwako..
1. πKujitambua( recognizing your own existance
also the existance of nature)
2. πKujua uwezo wako..(knowing your limititations and capabilities) hasa uwezo utokao ndani yako, (your cans and can’ts)
Na siku zote nguvu ya asili ya ndani ya mtu ndio inayompa mwanadamu nguvu ya kutamba duniani..achana na elimu yako, nazungumzia uwezo wa ndani ambao hakuna mwanadamu anaweza kuunyamazisha, na wala uwezo huo hauna limitations katika dunia…mfano uwezo wako wa kuongea, kufikiri, kuwaza, kuimba.
Sasa mwanadamu ameumbiwa tumaini ambalo liko ndani ya uwezo wake, uwepo wake na nguvu zake..ambalo tumaini hili likikosa rutuba hupotea..na ndipo hapo neno hili “I lost my identity” hutokea.
Miaka Fulani nilikuwa na uwezo mkubwa wa kukaa kimya, uwezo huo ulinipa nguvu sana na hekima hasa nilipokuwa katika kufanya maamuzi.
Na nilianzaga tu kwa kujiwekea ratiba ya kukaa kimya kwa muda flani…haikuchukua muda mrefu nikajikuta nimefanikiwa katika kukaa kimya
Sasa nikapenda nilivyo, na nikapenda ule uwezo wangu wangu wa kunyamaza pale ambapo nilitakiwa kusema…
Siku zikaenda, na mara nikaacha kufuata ile ratiba yangu ya kukaa kimya kwa muda… hasa wakati wa usiku.
Na mara nikajikuta nimebadilika.. mdomo ukawa mwepesi na ubongo ukawa mzito kufikiri…. Na baada ya hapo nilipoteza uwezo wangu mkubwa niliokuwa nao wa kukaa kimya ..
Kuna
tabia nyingi nzuri zinaweza kupotea kwenye Maisha yako kama hutatumia nguvu
kuzishikilia…na pengine kupotea kwa tabia
hizo kunaweza kushusha hadhi yako, au pengine uwezo wako wa kujiamini au
wakiroho..
Kuna
watu wamepata sifa kwa tabia flani flani tu, na mara wakajikuta wamepoteza sifa
hizo.. kitu ambacho kimezimisha mioyo yao kusimama tena…
π’Sio
rahisi kwa mtu kukueleza kwamba nimepoteza sifa Fulani…au sina uwezo tena wa
kufanya kitu flani… lakini ni hali ambayo inawapata watu wengi sana…
Ukipata hali hiyo..usiogope.. unaweza ukarudi katika hali yako ya mwanzo…nothing is impossible…unaweza kuanza upya….asili imetupa nafasi ya kuanza upya au kuunda kitu kipya.. mwanadamu anaweza ivyo vyote..Na Mungu yupo kutusaidia....USIOGOPE
πUjumbe wa makala hii, ni kukukumbusha tu kwamba jithamini, thamini thamani yako, pia uthamani huja katika kutambua uwezo wako wa asili.. tumaini la kweli huletwa na Mungu…hatakama hutaki kumtumikia Mungu una wajibu wa kumwamini na kumtumaini Mungu….π
Asante
na Mungu akubariki
its me, Angel Fabian ....
Comments
Post a Comment