Moyo wa Mtu ni Kama Kichaka


Mtu si kitu hata awe vile utakavyo, maana unaweza fanya kitu kuwa vile unavyotaka wewe...

mtu nnayemzungumzia hapa ni yule ambae ana utu ndani yake,
na utu huo ni upi, utu huu ni ule utu wa ndani ya mtu yaani nafsini mwake...

lengo langu si kukujulisha maana ya utu, ila ni kukukumbusha tu kuwa mtu ni mtu..


Tumekuwa tukiwapa nafasi na uthamani baadhi ya watu, na kuweka imani zetu juu yao, labda kwamba hawawezi kukosea, au labda mtu fulani hawezi kufanya jambo hili, au pia labda hawezi kushindwa..

hiyo imetupa tabu sana pale ambapo tumesikia au kuona tusivyovitarajia kwa watu hao,

Wengine hatuendi kanisani eti kwasababu mchungaji au padri ametenda dhambi. 
na wengine eti tumeshindwa kuendelea kwasababu fulani alishindwa,
eti fulani alisema ameshindwa kwahiyo me siwezi..
eti, kama yeye alishindwa me nawezaje..

Maana yaliopo sasa ni kunyoosheana vidole tuuu, eti fulani nae kafanya hivi, eti nae anaongea hivii..imani kwa Mungu imepungua eti tu kwasababu ya kiongozi mmoja wa dini...


kwani yeye sio mtu hata asishindwe...

kwani yeye ni nani hasa, hata asikosee...

Mtu, nia au utu wake huwezi tambua kwa yale tu unayoyaona nje, labda vitendo au maneno anayoongea...

maana siku hizi, hatuishi tena kulingana na vile vya ndani yetu, na bahati mbaya zaidi, tunaishi vile watu wanataka tuishe..
kwahiyo kutambua nia ya mtu si rahisi kwa akili za kibinaadamu..

mama yangu aliniambia...
moyo wa mtu ni kama kichaka, huwezi jua ndani yake kuna nini..

maana kila leo mazuri hutamkwa na wale wasio wazuri..na wengine wazuri wamekaa kimya wakati wengine wakitamka...
maana yake ni kwamba si kila asemaye zuri, ni mzuri...na si kila mzuri atasema au kufanya mazuri wakati wote..


  • kamwe usiweke mategemeo yako kwa huyo aitwaye mtu...
  • na wala usimwamini huyo mtu, Na kaa ukitegemea lolote kutoka kwake...


  • Usisahau kwamba kila umuonae, basi ana jambo jipya kwako.. mpe heshima zake na uende zako...
  • hata yule umuonaye si wa thamani tena mbele yako, nae ana jambo jipya kwako...
  • jifunze, upite kule.....


Ni wewe pekee uliye muandishi wa kitabu cha maisha yako,
kuhusu mapito yako pia, ni wewe na Mungu wako, jirani yako au rafiki yako aliyeanguka leo, wala hana cha kukusaidia kufika unapopaswa kufika, zaidi tu, umshukuru maana hilo ni funzo kwako.....

kumbuka watu huanguka na kusimama tena.
na akisimama tena, usijedhani kwamba atakuwa yule yule... aliyesimama atakuwa na nguvu kuliko yule aliyeanguka....

Mungu atusaidie.



Comments

Popular Posts