YESU NA KANISA LETU

Nilienda siku moja katika kanisa moja kubwa sana lenye kufahamika sana jijini Dar es salaam, Ilikuwa ni mara yangu ya pili mimi kukanyaga katika lile kanisa baada miaka  mingi kupita,
kanisa lilifurika watu wengi jumapili ile, na watu wengi walionekana kuwa na shauku ya kupokea miujiza yao...

Nyuso za watu wengi zilionyesha kukata tamaa na kuchoshwa sana na hali ya ugumu wa maisha, Wengine waliwaleta wagonjwa wao pale kanisani na wengine walikuja kwa ajili ya kutatuliwa matatizo yao binafsi.....

Madhabahu ya kanisa lile ilikuwa nzuri na ya kupendeza, vitambaa vyake vilikuwa vikimetameta, ilikuwa ni raha sana ukiangalia madhabahu ile, na ukiangalia hata wahudumu walikuwa wamevalia mavazi mazuri ikiashiria uzuri wa hali za maisha yao.
mchungaji mkuu alivalia vazi zuri kubwa la kumetameta kiasi kwamba alikuwa akionekana kanisa zima hata ukiwa mbali..

Ibada iliendelea waimbaji wazuri waliitwa wakaimba watu wakafarijika na kufurahi sana ile siku
Basi mchungaji akapanda madhabahuni kwa ajili ya neno....


Asilimia 90 ya ibada nzima ilikuwa ni watu kuhaidiwa kupokea miujiza yao ikiwemo kupata magari, nyumba nzuri za kuishi, kupona magonjwa...Na watu walisisitiziwa kuamini ili ya kupokea miujiza yao.

Ibada iliendelea, huku mafuta ya kiupako yakiwa yanapitishwa kwa ajili ya kuuzwa...mafuta hayo yalikuwa yakiondoa magonjwa na matatizo kwenye biashara na nyumba yako

Sadaka za kila aina zilitolewa, na niliona watu wakienda kutoa sadaka zaidi ya mara 3 mara 4, wakiamini kupokea majawabu ya shida zao...

Macho yangu yaliona pia hata wale ambao walikuwa wakionekana kutokuwa na uwezo kushiriki kutoa sadaka zile kwa zaidi ya 3

Niliona pia watu ambao walikuwa wakishangaa shangaa tu kanisani wakati tukiimba, wao wamekaa, tukiambiwa sema maneno haya, wao walikuwa kimya wakishangaa, nilishuhudia wengine ambao ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushika biblia

sikwenda kwa ajili ya kuangalia hayo, ila nilijikuta nikiangalia hayo yote wakati ibada inaendelea.....

Ugumu wa maisha na shida mbalimbali imekuwa  sababu ya watu kuhudhuria makanisani wakitegemea kupata miujiza na pesa, na wengine ndoa zao na familia zao hazina amani.... na wamekuwa wakitafuta majawabu kwa na,na zote, kama kwenda kwa waganga na wengine wakanisani....


Mungu anasema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha...lakini pia MUNGU anasema tusiipende dunia na mambo yake, haha Isaya pia inatuambia ulimwengu unaomboleza, unazimia, inasema ulimwengu unadhoofika.. maana yake ni kwamba tusiwe watu wakupenda ulimwengu..

zaburi 17:14,15 inasema
ee Bwana kwa mkono wako uniokee na watu, watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako, hushiba wana huwaachia watoto wao akiba zao..bali mimi nikutazame uso wako katika haki, namkapo nishibishwe kwa sura yako..

Sisemi tuwe maskini na sisemi tusiwe watafutaji...biblia inasema tafuteni ufalme wa Mungu hayo mengine yote mtazidishiwa..
biblia inasema 1samweli 2:7 Bwana hufukarisha mtu nae hutajirisha, hushusha chini, tena huinua juu. 
Kumbukumbu la torati 8:18 bali utamkumbuka Bwana Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo.

Nguvu na uwezo wa kumiliki ni MUNGU anatoa kwa watu wake na anasema katika zaburi 49:16,17 Usiogope mtu atakapopata utajiri na fahari ya nyumba yake itakapozidi maana atakapokufa hatachukua chochote utukufu wake hautashuka ukimfuata.

Tumekuwa busy kwenye kufikiria jinsi ya kupata pesa kirahisi na kufanikiwa kwa haraka bila kumkumbuka ambaye anakupa nguvu ya kumiliki.....
Kutokufanikiwa katika mambo yetu ya kimaisha, umaskini, magonjwa, mahusiano na familia vimetufanya tusahau uwepo wa MUNGU na kutufanya kutafuta namna za kishetani kuweza kufanikiwa..

Namna na mienendo ya Dunia ya sasa, inatupa ugumu hata wa kuweza kuaminana sisi kwa sisi...watu wamekuwa wakiamini makanisa na wachungaji kuliko wanavyomwamini MUNGU...watu hawana hofu ya MUNGU...

kikubwa MUNGU anatamani, ni wewe kumjua, kumpenda na kumtumika, ni wewe kumwabudu na kusifu.... ni wewe kujitoa kwa ajili yake, ni wewe kumwamini kwa moyo wako yote. katika maisha yako, familia yako, Mungu awe tegemeo lako... na hautabaki kama ulivyo, utajiri na fahari zitakufata na utaitwa mbarikiwa.

Mungu akubariki sana, nategemea baada ya kusoma hapa hautokuwa mkristo wa kufuata dini au wachungaji nategemea wewe utakuwa mwalimu wa maisha yako mwenyewe kupitia biblia na roho mtakatifu ndani yako..nategemea utatengeneza dunia yako na MUNGU , na nategemea utawavuta watu wa dunia katika ulimwengu wako.

AMEN

Comments

Popular Posts