MAISHA NA TANZANIA

Maisha ni mkusanyiko wa matukio vipindi vyote vya maisha ambavyo mtu binafsi ameweza kuvipitia tangu alivyozaliwa mpaka sasa alipo na umri aliokuwa nao
Kuishi katika jamii na aina ya watu wa kitanzania kumenipa maana hiyo ya maisha...nikimaanisha kwamba kila mtu ana maana yake na jinsi yake ya maisha...
Imenifundisha kuwa kila mwanadamu ana maisha yake...ambayo ni tofauti na mwingine na ndio hapo utapata mitazamo tofauti juu ya maisha...

Inanipa wakati mgumu sana kufikiri jinsi gani unaweza kuishi maisha yako kwenye jamii ya watu zaidi ya milioni ambao kila mtu pia anaishi maisha yake....

Kuna watu ambao Mungu amewapa neema ya kutoonja hata tone la shida tangu wamezaliwa hadi kufa...na kuna wengine sio tu kuonja ...ila wanapata shida tangu mwanzo wa kuzaliwa au mwisho wao na ndio hao watumishi wazuri wa Mungu...

Kuna wengine wanafanikiwa sana kimasomo...ila kuna wengine wanakesha usiku kucha kusoma lakini hawafanikiwi...

Kuna wengine wanapata shida pale tu wanapokaribia kufanikiwa...na wengine hata bila kufanikiwa shida huwafata...

Mbali na kusudi au mpango wa Mungu katika maisha ya kila mtu...katika jamii hii ya kitanzania, nimejifunza kitu kikubwa hasa umuhimu wa kuwa na uwezo wa kuongea na Mungu...ili kujua ni nini ameanda kwa ajili ya maisha yako..

Unapoishi mahali popote au unapokuwa mahali popote ...jaribu kujifunza lakini usiige ...kuwa tayari kusikiliza au kujua miitikio ya watu juu ya jambo fulani..au watu wana maoni gani au sura gani juu ya vitu fulani...hiyo itakusaidia kupata njia nyingi ambazo zitakusaidia kukabiliana na changamoto na kujua mfumo au njia za kusaidie eneo ilo...

Nimepata shida kidogo katika maeneo ya kazi katika jamii yetu hii ya kitanzania....eti tunachangua kazi...eti tunataka kazi zenye mishahara mikubwa ..eti atutaki umasikini kwahiyo biashara ndogo ndogo hatufanyi na wengine wanakataa kazi...

Kijana mtanzania uliye soma au usiyesoma....tumia ubongo kupambanua njia za kujikwamua kimaendeleo...wanasemaga siharakie maisha....wanasemaga pia...hata mbuyu ulianza kama mchicha...hakuna mafanikio makubwa ambayo utaweza kuyapata kwa njia rahisi...mtumikie Mungu na ufanye kazi.....

kijana mtanzania...maamuzi yako ya leo ndio maisha yako ya kesho....Mungu alitupa akili tuweze kuitumia kufanya maamuzi...tumia akili yako vizuri fanya maamuzi mazuri...kupikia bidii yako Mungu nae atakubariki...

Mtu wa Mungu...tumika na utumikie ...usitafute ufalme ndani ya dunia iliyotawaliwa na shetani..mpe Mungu nafasi aweze kutumika na wewe katika kipindi chote cha maisha yako kwasababu wewe ni mfalme katika ufalme wa Mungu...sio duniani...

Napenda nchi yangu...lakini ujana wa nchi yangu mbovu katika nyanja nyingi....
Tupende kujifunza tanzania...vijana na watoto wa Tanzania...tumika pale ulipoitwa na Mungu kutumika ...utafanikiwa...
 dedication to somebody..
God bless you all 
In the mighty name of Jesus...
 
Kwenye hii post jifunze vitu vifuatavyo..

1) kila mtu ana maisha yake mungu amempa ...usijilinganishe...wala usiige maisha ya mtu mwingine ishi yako

2)usichague kazi....fanya kazi kama unataka kufanikiwa

3) Mtumikie Mungu...na tafuta ufahamu juu ya jinsi ya kuongea na Mungu kwa habari ya maisha yako...
 
4)penda nchi yako...😊


Karibu tena

Comments

Popular Posts