Use faith as a bridge to your success

Imani...
Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo ni bayana na mambo yasiyoonekana.....

   Siku moja nilikuwa nafanya mtihani wangu wa mwisho wa semister, mitihani haikuwa mirahisi, vitu vilikuwa vingi kwangu...na moyoni mwangu nikadhamiria kutokupata supplementary na nafsi yangu ikawa inaniambia mambo yote yanawezekana kama nikiwa na imani.....
   Nilikuwa napita kwenye kipindi kigumu, nikiwa na maswali mengi..kama "nifanyaje imani yangu ikue ili nisifeli,..niki muomba Mungu sana nisipite huko na niwe na imani..........
    Lakini Mungu aliniaidia sikupata supp hata somo moja...kitu ambacho kwa uhalisia isingewezekana...
  Kutoka hapo imani yangu ikaongezeka sana kwa mungu..upendo wangu kwake ukazidi kuongezeka siku hadi siku....
   Namshangaa shetani katika kipindi hicho Ambacho nazidi kumpenda Mungu, yeye akazidi kujionyesha dhahiri hadi nikaanza kumtambua kwa macho....
       Kitu ambacho napenda nikushirikishe ni hiki...
Shetani ni adui wa roho na nafsi zetu...hua anafanya namna zote kuharibu nafsi na utulivu wa roho zetu ili aweze kukuweka mbali na Mungu...
     Jambo moja tambua...ni kwamba Mungu anatupenda sana...na hataki hata mmoja wetu apotee...ila anatamani tumwamini...wingi wa imani yetu kutasababisha Mungu ajidhihirishe kwenye maisha yetu
Tumwombe Mungu atupe imani hata ya kunyanyua milima...atupe imani ili shetani asitushinde...atupe imani ili tuweze kufanikiwa kwenye maisha yetu....

 It is hard to keep the faith in difficult situations. It is hard not to lean on your own thoughts and feelings at times. But we always must remember that the Lord knows what is best and will help us avoid any snares on the path we are on. We must always put our faith in Him when it comes to the path He puts us on.
Nakupenda sana...karibu tena katika kusoma post nyingine na Mungu akubariki
Nakutakia kukua kwema kwa imani yako ili tumwangushe shetani katika maisha yetu...
Amen
God bless u

Comments

Post a Comment

Popular Posts